
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo amefanya kampeni za nyumba kwa nyumba kutafuta kura za Dk. Samia Suhulu Hassan ili aendelee kuwatumikia Watanzania.
Kampeni hizo zimefanyika kwenye Kijiji cha Kakobe, Kata ya Kazunzu kabla ya uzinduzi wa kampeni kwenye kata hiyo zilizofanyika kwenye Kijiji cha Nyambeba jimbo la Buchosa.
Shigongo amewaomba Wanabuchosa washirikiane kwa pamoja kutafuta kura za rais kwa lengo la kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!