
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia sakata la Zuchu na mwanadada Rita mitandaoni.
Anasema Zuchu hastahili kabisa kurushiana maneno na mtu ambaye sio level yake, kikubwa ni kujishusha Ki-Brand.
Anasema Zuchu kwa sasa anavipa nafasi vitu visivyo vya msingi na ndio maana anatoka kwenye Focus ya kimuziki na hata ukifuatilia kwa Numbers ameshuka.
Zuchu alikuwa anatengeneza Viewres wengi sana kupitia ngoma zake mpaka kufikia hatua kusema yupo tayari kushindana na wasanii wa kiume.
Kuna namna Zuchu anatakiwa kuitumia nafasi ya kuwa karibu na Diamond kimuziki zaidi na sio kwa vitu visivyo vya msingi ambavyo havimjengi bali vinambomoa.
Ukija na nje ya Mipaka ya Tanzania kuna namna Zuchu hafanyi vizuri kama mwaka mmoja uliopita na hiyo ni kwa sababu ameondoka kwenye focus ya muziki ambayo ilikuwa inamfanya awe na muda wa kufanya Promo ya ngoma zake.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!