Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

CCM Kuanza Harambee ya Bilioni 100 Kesho, Rais Samia Kuongoza Uzinduzi

  • 12
Scroll Down To Discover

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kuwa chama chake kimepanga kukusanya Shilingi Bilioni 100 kupitia harambee ya kitaifa itakayozinduliwa rasmi kesho, saa 11 jioni, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Akizungumza leo Agosti 11, 2025, na wahariri pamoja na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo za CCM Makao Makuu, Lumumba, jijini Dar es Salaam, Dkt. Nchimbi alisema hatua hiyo imechochewa na hamasa kubwa ya wanachama wa CCM kutaka kuchangia kampeni za uchaguzi.

“Kwa wakati ule kulitokea hamasa kubwa kwa wanachama wa CCM kutamani kuchangia michango ya kampeni. Kutokana na hamasa hiyo, sisi kama Kamati Kuu tumeamua sasa kuwashirikisha wanachama wetu katika uchangiaji kesho saa 11 jioni katika ukumbi wa Mlimani City,” alisema Dkt. Nchimbi.

Ameweka bayana kuwa lengo la kukusanya ni Shilingi Bilioni 100, akisisitiza kuwa michango hiyo inakaribishwa pia kutoka vyama vingine vya siasa.

“Wanasiasa kokote walipo wajue hiyo ndiyo target tunayokusudia. Kuhusu vyama vingine, tutafarijika sana vikichangia, kwa sababu haihitaji ushahidi wa kipolisi kujua CCM inatumikia Watanzania na vyama vingine vyote,” aliongeza.

Kuhusu udhibiti wa fedha haramu, Dkt. Nchimbi alisema CCM haitajihusisha na uchunguzi wa fedha hizo, kwani si jukumu lake.

“Jitihada yetu kubwa sisi kama CCM ni kujiepusha kuwa Serikali, kwa hiyo sisi siyo taasisi ya uchunguzi wa fedha haramu. Wenye kazi yao wataendelea kutafuta fedha hizo, sisi tutaendelea kufanya kazi ya siasa,” alifafanua.

Harambee hiyo itakayolenga maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, itapambwa na uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.



Prev Post CRDB Yazindua Hatifungani ya Kwanza Isiyo na Riba kwa Wawekezaji wa Kiislamu
Next Post Wakulima Wabenkika Kidijitali Mpaka Shambani na Azania Bank Nanenane 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook