Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

HUKO SIMBA MAMBO BADO AISEEE…..ATEBA AKIPIGWA BEI TU…CHUMA HIKI KINATUA CHAP…

  • 46
Scroll Down To Discover

KIKOSI cha Simba kinaendelea kujifua kikiwa kambini jijini Ismailia, Misri kujiandaa na msimu mpya wa mashindano na kuna kazi ya maana inaendelea kufanywa na kocha Fadlu Davids akisuka kikosi kwa akili na hesabu zake na habari mpya ni mipango yake ya kuunda safu mpya ya ushambuliaji.

Kocha Fadlu anayesimamia usajili wa kikosi hicho, amejulishwa kwamba kuna uwezekano wa kumuuza straika aliyemaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 13, Lionel Ateba kufuatia uwepo wa ofa zake mbili mezani kwa mabosi wa klabu hiyo, lakini kuna moja ndio angalau inaonekana kuwa siriazi ya kutaka kumbeba nyota huyo raia wa Cameroon.

Kama Simba itafanya biashara hiyo ya kumuuza Ateba, basi Fadlu ameshaandaa majina mawili ambapo mmoja  akisubiri kupewa nafasi ya Mcameroon huyo mwenye mwili jumba.

Ipo hivi. Simba imefanya mazungumzo na mshambuliaji Privat Djessan Bi ambaye alimaliza msimu uliopita akiitumikia klabu ya Zoman FC ya Ivory Coast ambayo ndio iliyowauzia Yanga straika Celestin Ecua aliyekuwa akikipiga kwa mkopo ASEC Mimosas na kumaliza na mabao 15 na asisti 12.

Faili la Djessan lipo katika mikono ya Fadlu akikubali uwezo wake, lakini anachosubiri kocha huyo Msauzi ambaye ni mshambuliaji wa zamani ni uhakika wa biashara ya mauzo ya Ateba tu ili amshushe staa mpya.

Djessan msimu uliopita akiwa na Zoman, alihusika katika mabao 12 akifunga saba na asisti tano, lakini ikielezwa wakati akicheza sambamba na Ecua, ndiye aliyekuwa akimtengenezea na kumlisha mipira aliyokuwa akiitia kambani, kutokana na uwezo wake wa kutumika kama mshambuliaji namba mbili.

Ubora wa Djessan ni kwamba anaweza kucheza kama mshambuliaji na pia kama kiungo mshambuliaji akiwa na ujuzi wa kufunga mabao.

Inaelezwa Djessan anacheza kwa ustadi mkubwa kama namba 10 na pia kutokea pembeni na kutoa pasi zenye macho kwa wenzake mbali na kufunga, na inadaiwa mazungumzo ya kutakiwa kutua Msimbazi yalishaanza mapema, ingawa tatizo ni idadi ya nyota wa kigeni ndani ya Msimbazi.

Simba tayari imeshakamilisha idadi ya wachezaji 12 wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za usajili, ambao ni kipa raia wa Guinea, Moussa Camara, mabeki Chamou Karaboue (Ivory Coast), Rushine de Reuck (Afrika Kusini) na Neo Maema anayesubiri utambulisho.

Pia kuna viungo ni Allasane Kante (Senegal), Mkenya Mohamed Bajaber, Mzambia Joshua Mutale, Ellie Mpanzu, Jean Charles Ahoua, Jonathan Sowah, Steven Mukwala na Ateba.

Hata hivyo, taarifa nyingine zinasema kuna uwezekano Joshua Mutale akaondoka kikosini kwa dili zilizopo mezani kwa mabosi wa Simba kama ilivyo kwa Ateba, Steven Mukwala na Jean Charles Ahoua, hivyo kumrahisishia Djessan kutua Msimbazi na kuanzisha ligi ndogo na Ecua aliyepo Yanga.

The post HUKO SIMBA MAMBO BADO AISEEE…..ATEBA AKIPIGWA BEI TU…CHUMA HIKI KINATUA CHAP… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KWA MKATABA HUU WA YANGA KWA TSHABALALA….SIMBA WALISTAHILI KUKIMBIA…ATAKUNJA BIL 1.2
Next Post NAFASI YA KUSHINDA UNAYO MERIDIANBET LEO…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook