INAELEZWA kuwa winga chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids ndani ya kikosi cha Simba SC, Ellie Mpanzu yupo kwenye rada za RS Berkane,Waarabu wa Morocco.
Mpanzu ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa tegemeo katika kikosi cha Simba SC msimu wa 2024/25 kwenye anga la kimataifa na kitaifa.
Ndani ya ligi rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 17 kati ya 30. Ikumbukwe kwamba Mpanzu aliibuka ndani ya Simba SC kwenye dirisha dogo la usajili.
Simba SC ikiwa imefunga mabao 69 kahusika kwenye mabao 7, akifunga manne na kutoa pasi tatu. Ni dakika 1,239 alikomba uwanjani.
Ikiwa RS Berkane wataipata saini yake, Simba SC itakuwa na kazi kusaka winga mwingine ambaye atakuja katika kikosi hicho.
The post ISHU YA MPANZU KUTAKIWA NA WAARABU …UKWELI WOTE HUU HAPA… appeared first on Soka La Bongo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!