

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Julai 8, 2025 amepokea Tuzo Maalum ya Heshima ya ‘Power of 100 Women’ kutoka kwa Uongozi wa Access Bank Group, ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika kuleta mageuzi ya kijamii na kiuchumi barani Afrika, hususan katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi.
Tukio hilo limefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo tuzo hiyo ilikabidhiwa rasmi kwa Rais Samia na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Access Tanzania, Ndugu Protase Ishengoma, kwa niaba ya uongozi mzima wa Access Bank Group.
Tuzo ya Power of 100 Women hutolewa kila baada ya miaka mitano kwa lengo la kutambua, kusherehekea na kutia moyo wanawake wa Kiafrika wanaoleta mabadiliko makubwa katika mataifa yao, na kuchochea kizazi kipya cha wanawake viongozi barani Afrika.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!