
Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar kimeendelea kupoteza wanachama na viongozi wake ambao kati yao wametangaza kuhamia CCM huku ikitajwa kuwa wengi wao wapo mbioni kufanya hivyo.
Wanachama na viongozi wa kwanza kufanya hivyo ilikuwa katika viwanja vya Mauani Kiwani, Mkoa wa Kusini Pemba wakati wanachama wa ACT Wazalendo 2,439 waliporudisha kadi za chama hicho na CCM.
Tukio hilo ilikuwa wakati wa mapokezi ya Rais Hussein Mwinyi, viwanja vya Mauwani Kiwani, Mkoa wa Kusini Pemba, 15 Februari mwaka huu, baada ya Mkutano Mkuu wa dharula wa CCM kumtangaza kuwania Urais wa Zanzibar 2025.
Mkutano huo pia ulimtangaza Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ndiye mgombea wa chama hicho wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mei 17 mwaka huu katika Viwanja vya Mpendae, katika mkutano wa hadhara Rais Dkt. Mwinyi, amewapokea vigogo wawili wa chama hicho waliotangaza kuhamia CCM.
Vigogo hao ni Katibu wa Mipango na Uchaguzi, Ngome ya Vijana ACT Wazalendo, Hamad Mbarouk Juma na aliyekuwa Naibu Waziri Kivuli, Utumishi wa Umma katika Baraza la Wawakilishi, Halima Abbas Mohammed.
Kiongozi huyo wa ngome ya vijana, anasema kuna vijana wengi wanatoka ACT Wazalendo kwenda CCM hivyo akamuomba Makamu Mwenyekiti na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwapokea.
Alisema wanakuja CCM baada ya kubaini ukweli wa ile ambacho kinafanywa na Rais Dkt. Mwinyi hivyo, ACT haina hoja kwa wananchi.
Pia alisema ndani ya ACT Wazalendo watu wamejengewa mazingira kutakiwa kutokuhoji lolote jambo linalofanywa na viongozi na ndio maana wanachama hawaongezeki.
Alibainisha kuwa kuna itikadi ya chama isemayo ‘umeona pinga, hujaona pinga’ na ndio maana sura katika safu za wanachama na viongozi hazibadiliki. “Ngumu sana kuwashawishi vijana kujiunga na ACT Wazalendo na kuna viongozi wamekataliwa na wanajua, wamekataliwa lakini hakuna wa kusema.” Alisema Mbarouk, kundi hilo la vijana wanatoka ACT na kuja kujiunga na CCM kutokana na mateso wanayopitia toka wakiwa Chama cha Wananchi (CUF).
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!