Banda la Bodi ya Bima ya Amana katika Maonesho ya Kilimo, MIfugo na Uvuvi (Nanenane) yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma limeendelea kutembelewa na wananchi mbalimbali wanaofika katika maonyesho hayo ili kupata uelewa namna Bodi hiyo inayoendesha shughuli zake katika kukinga amana za wateja katika benki na taasisi za fedha.
Meneja Uendeshaji wa DIB, Bw. Nkanwa Magina pamoja na maofisa mbalimbali wa taasisi hiyo wanaendelea na utoaji elimu kwa wananchi ili kuhakikisha DIB inafahamika zaidi kwa wananchi na majukumu yake katika kuhakikisha elimu hiyo itawafika watanzania wengi nchini.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!