Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Yanga Yaanza Mazungumzo na Dickson Job Kuhusu Mkataba Mpya

  • 53
Scroll Down To Discover

Inaelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Yanga SC umeanza mazungumzo rasmi na beki wao tegemeo Dickson Job, kuhusu kuongeza mkataba mpya ili aendelee kusalia ndani ya klabu hiyo kwa msimu ujao.

Job ambaye alikuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Yanga SC msimu wa 2024/25, ameonesha kiwango bora na uimara wa hali ya juu, hali iliyowafanya mabosi wa timu hiyo kutaka kumshikilia zaidi.

Katika msimu huo uliomalizika kwa mafanikio kwa Yanga SC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa kujikusanyia pointi 82 kwenye mechi 30, Job alicheza mechi 26 kati ya hizo, akicheza dakika 2,340 kati ya jumla ya dakika 2,700, na kukosa mechi nne pekee.

Ingawa msimu wa 2023/24 aliibuka mfungaji wa bao la kwanza la Yanga kwenye ligi, msimu huu wa 2024/25 amemaliza bila kufunga goli lolote lakini mchango wake kwenye safu ya ulinzi umebaki kuwa wa thamani kubwa.

Chanzo cha karibu na klabu hiyo kimeripoti kuwa uongozi wa Yanga SC umeshaanza mazungumzo ya kumshawishi Job kuongeza mkataba, huku wakionesha dhamira ya dhati ya kuendelea kunufaika na huduma yake.

Ofisa Habari wa Yanga SC, hivi karibuni alinukuliwa akisema:

“Ikiwa mchezaji tunahitaji huduma yake basi tutaweka hela ili abaki. Unakumbuka kuhusu Aziz Ki? Kuna timu zilikuwa zinamuhitaji lakini tukamuongezea mkataba.”

Kauli hiyo inazidi kuonesha kwamba Job ni miongoni mwa wachezaji walioko kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo.

Mashabiki wa Yanga SC wanaendelea kusubiri kwa hamu matokeo ya mazungumzo hayo, huku wengi wakimtamani Job kuendelea kuwa ngome imara ya safu ya ulinzi ya Wananchi kwa misimu ijayo.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.



Prev Post Makamu wa Rais Aungana na Wakatoliki Kuuadhimisha Jubilei ya Parokia Dodoma
Next Post Baba Mzazi wa Mbwana Samatta Afariki Dunia – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook