Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Tantrade Yaadhimisha Programu ya Urithi Wetu kwa Kuwakutanisha Wanafunzi

  • 46
Scroll Down To Discover

Dar es Salaam 6 Julai 2025: Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) imeadhimisha programu ya Urithi wetu kwa kuwakutanisha wanafunzi kutoka mikoa mitano Tanzania Bara na Visiwani kwa lengo la kuwajengea moyo wa uzalendo kupitia uelewa wa historia na maendeleo ya Taifa.
Miongoni mwa mikoa waliotokea watoto hao ni pamoja na Kigoma, Mbeya, Kisarawe, Unguja na Pemba na kupelekwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo SGR, Tanzania airport Authority pamoja na SIDO hii ni kuwajenga watoto pindi wanapokuwa baadae na kumaliza darasa la saba kuchagua nini anaweza kufanya.
Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam,Afisa Biashara wa Tantrade,Farhia Mohamed, alisema programu hiyo ya Sabasaba Urithi wetu ni nzuri na wanatamani kuendelea nayo ili kuwa mabalozi wazuri wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na kwa nchi.
Alisema programu hiyo inamjenga mwanafunzi kusoma kwa vitendo zaidi na sio nadharia kama wanavyosoma Darasani na kumjenga kutokusahau historia ya Tanzania tangu alipokuwa Mkoloni Mjerumani,Muingereza hadi kupata uhuru.
”Hii Programu ni Sabasaba Urithi wetu ambayo inaratibiwa na Tantrade chini ya Mratibu Mkuu Mkurugenzi wa Tantrade na sasa hivi tupo mwaka wa nne tangu ianze na lengo kuu ni kuwarithisha watoto wa kitanzania kuijua kwa undani siku ya Sabasaba ni nini,hivyo tunawpatia historia mbalimbali kwa kuwatembeza ili waweze kusoma kwa vitendo.
”Mwanafunzi anaposoma Darasani na kuja hivi kujifunza kwa vitendo na kuona inamjenga na hataweza kusahau maishani mwake na kuwa balozi mzuri hata akienda nchi nyingine ataweza kueleza Tanzania inahistoria gani,”alisema.
Kwa upande wake Mwalimu Bertha Mtanda kutoka Mkoani Kigoma,alisema ziara hiyo inalenga kuwajenga wanafunzi wao kujua vizuri historia ya Tanzania tangu wakoloni wote.
”Nimewaleta hapa watoto kujifunza na sisi walimu pia tumekuwa tukijifunza kupitia programu hii hivyo tunaishukuru Serikali yetu kwa kuwa imetupa nafasi ya kuwaleta watoto ili waweze kujifunza mambo ya historia ya taifa letu,”alisema.
Mmoja wa wanafunzi hao,Elizabeth George kutoka Shule ya Sekondari ya Jokete Mwegelo alisema kupitia programu hiyo wameweza kujifunza vitu mbalimbali kabla ya Ukoloni,baada ya Ukoloni na hadi Uhuru.
”Kitu cha muhimu nimekiona kwangu ni kuona gari la kwanza alilotumia Mwl.Nyerere hadi la mwisho,kiukweli tumefurahi na kujifunza vitu vingi kuhusu historia kwani historia ni somo mojawapo tunalosoma shuleni na itatusaidia kutumia kujibu maswali katika somo la historia ,”alisema.



Prev Post Furahia Promosheni ya Wild White Whale Ukiwa na Meridianbet
Next Post Mtoto wa Mzee Samatta Azungumzia Chanzo cha Kifo cha Baba Yao – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook