Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kesi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini CHADEMA Yaahirishwa Mpaka Julai 10

  • 51
Scroll Down To Discover

Leo Juni 24, 2025 Kesi namba 8323/2025 ambayo imetoa zuio la muda kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuendesha shughuli za kiutendaji na oparesheni, imeahirishwa tena hadi Julai 10, 2025. Sababu ya kuahirishwa kwa kesi hiyo ni kutokuwepo kwa Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza shauri hilo, ambapo imeelezwa kuwa ana majukumu mengine.

Kesi hiyo ilitarajiwa kusikilizwa leo, Juni 24, 2025, katika Mahakama Kuu baada ya kufunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa chama hicho.

Wakili wa utetezi, Hekima Mwasipu, akizungumza baada ya kesi kuahirishwa, alisema kuwa Jaji hakuweza kufika mahakamani kutokana na kuwa na majukumu mengine.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema kuwa walitarajia hoja ya kumtaka Jaji Hamidu Mwanga kujiondoa katika kesi hiyo ingesikilizwa leo. Aidha, alieleza kuwa chama kitaendelea kuchukua hatua za ziada za kisheria ili kuhakikisha Jaji huyo anaondolewa katika usikilizwaji wa kesi hiyo kwa msingi wa maslahi ya haki.

Shauri hilo liliwasilishwa na mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe, wakiomba Mahakama kuweka zuio kwa CHADEMA hadi kesi ya msingi itakapoanza kusikilizwa rasmi.

Stori: Elvan Stambuli | GPL

VITA ya ISRAEL na IRAN: DUNIA INAWEZA KUTIKISIKA BEI ya MAFUTA KUPAA – UCHUMI UTAYUMBA!



Prev Post Zaidi ya Bilioni 1 Kuwaniwa Kwenye Mashindnao ya Mystery Multiplier Drop
Next Post Waziri Mkuu Azindua Mitambo Ya Uchorongaji Na Vita Vya Utafiti Kwa Wachimbaji Wadogo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook