Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wapalestina 1,500 Wauawa Huko Ghaza Tangu Mei, Un Yalaani “Mtego Wa Kifo” Wa Misaada

  • 38
Scroll Down To Discover

Umoja wa Mataifa (UN) umesema Wapalestina 1,500 wameuawa huko Ghaza tangu Mei hadi sasa wakati wanahangaika kutafuta msaada wa kibinadamu.

Farhan Haq, Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa, amewaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya umoja huo mjini New York leo: “Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu inasema watu wengi wanaripotiwa kuuawa na kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na watu wanaotafuta chakula kwenye njia za msafara wa Umoja wa Mataifa na maeneo ya usambazaji misaada ya kijeshi. Karibu watu 1,500 wameripotiwa kuuawa tangu Mei”.

Tangu Mei 27, mpango uitwao wa utoaji misaada ulioratibiwa na Marekani na utawala wa Israel huko Ghaza, GHF umekosolewa vikali kuwa haufanyi kazi na vilevile ni “mtego wa kifo” kwa raia Wapalestina wanaokabiliwa na mateso ya njaa.

Hayo yanajiri katika hali ambayo Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali ya Palestina huko Ghaza ilitangaza jana Jumatatu kwamba utawala Israel umeruhusu malori 67 tu ya misaada tangu Julai 27, ikiwa ni asilimia 14 tu ya mahitaji ya kiwango cha chini kabisa ya kila siku kwa ajili ya eneo hilo ya malori 600.

Jeshi la utawala wa Israel chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu limekataa katakata hadi sasa wito wa kimataifa wa kusitisha mapigano na kuamua kuendeleza mashambulizi ya kinyama huko Ghaza, ambayo tangu Oktoba 7, 2023 hadi sasa yameshaua Wapalestina 61,000, nusu yao wakiwa wanawake na watoto. Vita hivyo vya kinyama na vya mauaji ya kimbari vimeliteketeza pia eneo hilo na kulifikisha kwenye hali ya baa la njaa



Prev Post ZAWADI PAPO HAPO NA MYSTERY MULTIPLIER KUTOKA MERIDIANBET….
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI LEO AGOSTI 06, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook