Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Aliyekuwa Mbunge wa CCM Mpina Aonekana ACT Wazalendo

  • 24
Scroll Down To Discover

Hatimaye aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa mkoani Simiyu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Luhaga Mpina ameonekana kwenye vikao na viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo huku duru za kisiasa zikieleza kuwa chama hicho kimeridhia mwanasiasa huyo kujiunga nacho ili kupeperusha bendera yake katika nafasi ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Mpina ambaye ameenguliwa na CCM katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea Ubunge anatajwa kuamua kubadilisha jukwaa la kufanyia siasa na sasa huenda akawa mgombea wa Urais kupitia ACT.

ACT Wazalendo inatarajiwa kufanya mkutano wake mkuu tarehe 6 Agosti 2025 kwa ajili ya kumpitisha mwanachama atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya Urais mwaka huu.

 



Prev Post Airtel Money Na Benki Ya I&M Wazindua Mpango Wa Elimu Ya Kifedha  Kuwawezesha Wajasiriamali Wanawake
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook