Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Serikali yapiga marufuku aina 15 za biashara kwa raia wa kigeni

  • 48
Scroll Down To Discover

Serikali imepitisha rasmi Amri ya Leseni za Biashara (Marufuku ya Shughuli za Biashara kwa Wasio Raia), 2025, ambayo inazuia raia wa kigeni kufanya shughuli mbalimbali za kibiashara nchini, ikiwa ni sehemu ya kulinda fursa za ajira na kipato kwa Watanzania.

Kwa mujibu wa amri hiyo, biashara ambazo sasa hazitaruhusiwa kufanywa na wageni ni pamoja na uuzaji wa bidhaa kwa rejareja, huduma za saluni, uhamishaji wa fedha kwa njia ya simu, Uanzishaji na uendeshaji wa redio na televisheni, uongozaji watalii, umiliki au uendeshaji wa mashine za kamari, isipokuwa kama zipo ndani ya kasino.

Aidha, amri hiyo inakataza wageni kumiliki au kuendesha viwanda vidogo, kufanya biashara za uwakala wa fedha, udalali katika sekta ya biashara na ardhi, na kushughulika na matengenezo ya simu za mkononi na vifaa vya kielektroniki, usafi wa majumbani, ofisini na mazingira, huduma forodha na usafirishaji, uchimbaji mdogo wa madini na ununuzi wa mazao moja kwa moja kutoka shambani.

Mamlaka za utoaji wa leseni zimetakiwa kutoendelea kutoa au kuhuisha leseni kwa wageni wanaojihusisha na shughuli hizo, huku hatua za kisheria zikiainishwa kwa watakaokaidi, ikiwemo faini ya hadi TZS milioni 10, kufutiwa visa na vibali vya ukaazi, au kifungo cha hadi miezi sita.

Kwa upande mwingine, Watanzania watakaobainika kuwasaidia wageni kuendesha biashara hizo nao watakabiliwa na adhabu ya faini ya milioni tano au kifungo cha hadi miezi mitatu.

Serikali imesema wageni waliokuwa na leseni halali kabla ya kuanza kutumika kwa amri hiyo, wataruhusiwa kuendelea hadi pale leseni zao zitakapomalizika muda wake.

The post Serikali yapiga marufuku aina 15 za biashara kwa raia wa kigeni appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post Benki Ya Absa Tanzania Na World Vision Tanzania Wakabidhi Mradi Wa Maji Safi Kwa Kijiji Cha Kwedizinga
Next Post Majaliwa: Actif 2025 Itoe Majibu Ya Changamoto Za Kibiashara Na Uwekezaji
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook