
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Jumanne Mabodo (30) kwa tuhuma za kumuua mama mkwe wake Kabula Masanja (50) kwa kumkata kwa panga nyumbani kwa marehemu, kijiji cha Chumwi, Wilaya ya Musoma, Julai 19, 2025.
Binti wa marehemu, ambaye ni mke wa mtuhumiwa, alijeruhiwa na anaendelea na matibabu.
Chanzo ni mgogoro wa kifamilia baada ya mke wa mtuhumiwa kudai kuwa mumewe ni mwizi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!