
Mtoto Ramin, mwenye umri wa miaka mitatu, ambaye aliripotiwa kupotea siku kadhaa zilizopita huku taarifa zake zikisambazwa kwa kasi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, amekutwa akiwa tayari amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia na majirani, mwili wa mtoto huyo umekutwa leo ndani ya kisima kilichopo nyumbani kwao, mkoani Tabora.
Tukio hili limetokea baada ya juhudi kubwa za kumtafuta mtoto huyo, juhudi ambazo zilijumuisha familia, majirani, na wananchi walioguswa kupitia mitandao ya kijamii kwa kusambaza taarifa za kutoweka kwake.
Hadi sasa, mamlaka za usalama zinaendelea na uchunguzi wa kina kubaini mazingira kamili ya tukio hilo. Ripoti rasmi kutoka Jeshi la Polisi inasubiriwa ili kutoa mwangaza zaidi kuhusu chanzo halisi cha kifo hicho.
Tukio hili limeibua majonzi makubwa kwa jamii ya eneo hilo na watumiaji wa mitandao waliokuwa wakifuatilia kwa karibu hatma ya mtoto huyo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!