Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Muuguzi wa India asubiri kunyongwa Julai 16

  • 37
Scroll Down To Discover

Nimisha Priya

Na mwandishi wetu, Elvan Stambuli

Nimisha Priya alihukumiwa kifo kwa mauaji ya mwanamume mmoja ambaye alikuwa mshirika wake wa zamani wa kibiashara, Talal Abdo Mahdi – ambaye mwili wake uliokatwakatwa uligunduliwa kwenye tanki la maji mnamo 2017.

Njia pekee ya kumuokoa muuguzi huyo ni kama familia ya Mahdi itamsamehe. Ndugu na wafuasi wake wametoa $1m (£735,000) kama diyah, au pesa ya damu, ili kulipwa kwa familia ya Mahdi.

“Bado tunasubiri msamaha wao au matakwa mengine,” mjumbe wa shirika linalomtetea aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza – BBC. “Tarehe ya kunyongwa ( Julai 16 mwaka huu) imewasilishwa na mkurugenzi mkuu wa mashtaka kwa mamlaka ya jela. Bado tunajaribu kumwokoa. Lakini hatimaye familia inabidi ikubali kumsamehe,” Babu John, mwanaharakati wa masuala ya kijamii na mjumbe wa shirikamoja linalopigania kumuokoa nesi huyo alisema.

Afisa katika wizara ya mambo ya nje ya India aliiambia BBC kwamba bado wanajaribu kuthibitisha maelezo hayo. Nimisha Priya alikuwa ameondoka katika jimbo la kusini mwa India la Kerala kwenda Yemen mwaka 2008 kufanya kazi ya uuguzi.

Alikamatwa mwaka wa 2017 baada ya mwili wa Mahdi kugunduliwa. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa amefungwa katika jela kuu ya Sanaa katika mji mkuu wa Yemen.

Alishtakiwa kwa kumuua Mahdi kwa kumpa “kiwango cha juu cha dawa za kumtuliza” na kudaiwa kuukatakata mwili wake baada ya kufariki dunia. Hata hivyo, Nimisha alikanusha madai hayo.

Mahakamani, wakili wake alidai kwamba Mahdi alimtesa kimwili, akampokonya pesa zake zote, akamnyang’anya pasipoti yake ya kusafiria na hata kumtishia kwa bunduki.

Muuguzi huyo alisema alijaribu kumpa dawa ya ganzi Mahdi ili tu kuchukua pasipoti yake kutoka kwake, lakini dozi iliongezeka kwa bahati mbaya.

Mnamo 2020, mahakama ya eneo hilo ilimhukumu kifo. Familia yake ilipinga uamuzi huo katika Mahakama ya Juu ya Yemen, lakini rufaa yao ilikataliwa mwaka wa 2023.

Mapema Januari mwaka huu, Mahdi al-Mashat, rais wa Baraza Kuu la Wahouthi, aliidhinisha kunyongwa kwake.

Mfumo wa mahakama wa Kiislamu wa Yemen, unaojulikana kama Sharia, unampa matumaini ya mwisho – kupata msamaha kutoka kwa familia ya mwathirika kwa kulipa pesa za damu.



Prev Post China Yatoa Onyo Kwa Marekani Kuhusu Ushuru Mpya – Yaapa Kulipiza Kisasi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook