Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Dkt. Samia Ashiriki Ufunguzi Wa Kanisa La Arise & Shine Kawe Dar -Live Video

  • 48
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akifungua hema la Kanisa la Arise and Shine linaloongozwa na Mtume Boniface Mwamposa, Kawe Jijini Dar es Salaam leo Julai 5, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 5, 2025 ameshiriki katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Kanisa la Arise and Shine, iliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe – Dar es Salaam.

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na maelfu ya waumini na viongozi mbalimbali wa dini, serikali na taasisi binafsi, Rais Samia alipokelewa kwa furaha na heshima kubwa, huku akitoa hotuba iliyojaa busara, mshikamano wa kitaifa na ujumbe wa amani.

Rais amelitakia kanisa hilo kila la heri katika safari yake ya kiroho na kijamii, akisisitiza umuhimu wa taasisi za kidini katika kuimarisha maadili, upendo na mshikamano wa kijamii, pamoja na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.

Viongozi wa Kanisa hilo wamemshukuru Rais kwa kuwa kiongozi wa kwanza wa kitaifa kuhudhuria tukio la aina hiyo, na wamempongeza kwa juhudi zake katika kuimarisha uhuru wa kuabudu na kuendesha Taifa kwa hekima.

Rais Samia akiwasalimia Waumini wa kanisa la Arise and Shine alipowasili katika hafla ya Ufunguzi wa Kanisa la Arise and Shine, Kawe Jijini Dar es salaam.
Rais Dkt. Samia akiteta jambo na Mtume Boniface Mwamposa mara baada ya kuwasili katika Ufunguzi Kanisa la Arise and Shine, Kawe Jijini Dar es salaam.
Rais Dkt. Samia akiwasalimia Waumini wa kanisa la Arise and Shine alipowasili katika hafla ya Ufunguzi wa Kanisa la Arise and Shine, Kawe Jijini Dar es salaam.



Prev Post Infinix Hot 60 Pro+ Inakuja na Wembamba wa 5.59mm, Kuweka Rekodi ya Kipekee
Next Post Gonsalva Mlemavu Aliyehitimu VETA Anayepingana na Kazi ya Ombaomba
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook