Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

HII HAPA SAFARI YA SOWAH KWENDA YANGA…MIPANGO INASUKWA ‘KIMLALO

  • 27
Scroll Down To Discover

JONATHAN Sowah mshambuliaji wa Singida Black Stars anatajwa kuwa kwenye mpango wa kutakiwa na Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.

Sowah alimpa tabu kipa namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra kwenye mchezo wa ligi walipokutana Uwanja wa KMC Complex kwa kumtungua bao moja.

Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 2-1 Singida Black Stars, Sowah alifunga bao lakufutia machozi mbele ya vinara wa ligi.

Taarifa zinaeleza kuwa mchezaji mwenyewe anapenda kucheza ndani ya kikosi cha Yanga SC jambo ambalo linatoa nafasi kubwa kwa mabingwa watetezi kuipata saini yake.

Mshambuliaji huyo anayevaa jezi namba 3 ndani ya ligi amefunga jumla ya mabao 11 akiwa ni miongoni mwa washambuliaji wenye mabao mengi licha ya kujiunga na timu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili.

Singida Black Stars ni nafasi ya nne kwenye msimamo ina pointi 53 safu ya ushambuliaji imefunga mabao 40 baada ya mechi 28 mchezo wao ujao ni dhidi ya Dodoma Jiji unatarajiwa kuchezwa Juni 18 2025 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

The post HII HAPA SAFARI YA SOWAH KWENDA YANGA…MIPANGO INASUKWA ‘KIMLALO appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post TAA Yawahakikishia Wananchi Uaminifu Katika Usimamizi wa Viwanja 61 vya Ndege Nchini
Next Post HII HAPA SAFARI YA SOWAH KWENDA YANGA…MIPANGO INASUKWA ‘KIMLALO
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook