

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa ametangaza kwa Vyombo vya habari kuwa Mabaraza yote ya Halmashauri yanapaswa kuvunjwa ifikapo Tarehe 20/06/2025.
Taarifa ya Waziri Mchengerwa imebainisha kuwa ukomo wa Kamati zote za Halmashauri zinazoundwa na Madiwani wa Halmashauri zote nchini utakuwa ni Tarehe 20/06/2025.
“Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika ndiye atakayekuwa Mwenyekiti wa mpito wa Halmashauri akisaidiwa na Wakuu wa Idara kama sehemu ya Kamati hadi hapo Uchaguzi utakapofanyika.” Imesema taarifa ya waziri Mchengerwa.
Kulingana na TAMISEMI, hakuna Diwani atakayeendelea na majukumu yake mara baada ya Tarehe 20/06/2026.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!