Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TRA Yawapa Siku 14 Watumishi Wapya Kuripoti Kazini

  • 27
Scroll Down To Discover

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda ametoa siku 14 kuanzia Juni 06.2025 kwa waajiriwa wapya wa TRA ambao ni watumishi wa serikali kuripoti kazini na kuanza kazi la sivyo nafasi zao zitajazwa na waliokosa nafasi ambao wapo kwenye kanzidata ya TRA.

Akifunga mafunzo ya awali kwa waajiriwa wapya 1,896 wa TRA katika viwanja vya Gofu Lugalo Jijini Dar es Salaam Juni 06.2025 Kamishna Mkuu Mwenda amesema watumishi hao 118 pamoja na wengine nane ambao bado hawajaripoti kazini, wanapaswa kuwa wameripoti ndani ya wiki mbili ili kazi ziendelee.

“Nyie mmepata kazi, lakini kumbe tayari mna kazi serikalini, nawapa wiki mbili muwe mmesharipoti la sivyo tutalazimika kuwachukua waliopo kwenye kanzidata ambao hawana kazi” amesema Mwenda.

Aidha amewaonya waajiriwa wapya waliopokelewa kazini kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na badala yake wachape kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anayo imani kuwa idadi hiyo kubwa ya waajiriwa wapya itakwenda kuleta mapinduzi TRA kwa kuongeza idadi ya walipakodi na makusanyo kwa ujumla.

Amesema Rais Samia aliamua kuongeza idadi ya waajiriwa wapya 300 na kufikia idadi ya sasa 1896 ili kuwezesha TRA kuendelea kufanya vizuri katika kukusanya kodi na kuonya kuwa wasije wakajiingiza kwenye vitendo vya uvunjifu wa maadili na kuharibu taswira nzuri ya TRA iliyojengwa kwa muda mrefu.

“Kupata kwenu nafasi ya kufanya kazi TRA kumetokana na sifa ya kila mmoja wenu, mtakuwa mashahidi, mchakato ulikuwa ni mgumu na makini, lengo letu lilikuwa ni kupata watu sahihi na mmepatikana, hivyo tunawadai uwajibikaji, iwapo watatokea watakaofanya uvunjifu wa maadili hatutawavumilia, tutawawajibisha bila kujali hali zao, mazingira waliyotoka wala sifa zilizowapa kazi”, amesema Kamishna Mkuu Mwenda.

Kamishna Mkuu Mwenda amesema ni jukumu la watumishi wa TRA kuongeza idadi ya walipakodi kwa kuwasajili walipakodi wengi zaidi ndiyo maana Serikali imeajiri idadi kubwa ya watumishi ili wawafikie walipakodi wengi zaidi katika pembe zote za Tanzania.



Prev Post Seneti ya Vyuo Dar: Zungu ni Kiongozi wetu, Tuko Tayari Kumsimamisha Tena
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook