Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Diamond amuoa Zuchu, asema “Siku Ikifika Nitawaambia Ilivyokuwa”

  • 29
Scroll Down To Discover

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu maisha yake ya ndoa kwa kusema wazi kuwa tayari alishawahi kuoa. Akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram leo, Juni 1, 2025, Diamond amewashangaza mashabiki kwa ujumbe mzito ulioambatana na picha zinazomuonesha akifunga ndoa na Msanii Zuchu

Katika ujumbe huo, Diamond alizungumzia changamoto ya kukabiliana na mitazamo hasi kutoka kwa watu, huku akieleza namna alivyojifunza hekima ya kukaa kimya licha ya kuwa na ukweli wake binafsi. Alieleza:

“Miongoni mwa vitu ambavyo nimejifunza ni ukomavu wa kukaa kimya… Ukomavu huu unahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Unahitaji kuwa na moyo wa subira, hasa pale mtu au watu wanapokupakazia jambo baya katika jamii, ilhali wewe unao ukweli wake lakini unatakiwa ukae kimya—usijibu—wakati ukweli unao ndani yako.

Kwa kweli, si jambo jepesi. Linahitaji ustahimilivu wa hali ya juu sana. Siwezi kusema kwamba nauweza sana, lakini namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia hekima hiyo kwa kiwango chake. Nimekuwa nikiishi hivyo kwa muda mrefu—kukaa kimya kila anapojitokeza mtu kusema jambo lolote dhidi yangu.

Ndio maana hata mahojiano nimekuwa nikiyaepuka siku hizi. Ingawa si jambo rahisi, faida yake nimeiona na ni kubwa sana. Maana vita vyako vinapiganiwa na Mwenyezi Mungu, na hiyo inakufanya uwe mshindi kila siku.”

Katika kile kilichoonekana kama sehemu ya mwisho ya kuficha jambo hilo, Diamond aliandika:

“Najua kila mmoja wenu ana picha tofauti kabisa kuhusu Diamond Platnumz na suala la kuoa. Ila leo nataka niwaambie kitu kimoja: Huyu Diamond Platnumz alishawahi kuoa, na kuna siku nitawaeleza ilikuwaje.”

Kauli hiyo imethibitishwa pia na mama yake mzazi, Bi Sandra (Mama Dangote), ambaye aliposti video ya hafla hiyo ya ndoa na kuandika:

“Alhamdulillah limepita salama. Hongera Mwanangu Naseeb Kichwa na Mkeo Zuhura.”

Ujumbe huo wa Mama Dangote umeondoa sintofahamu ya muda mrefu miongoni mwa mashabiki kuhusu uhusiano kati ya Diamond na msanii Zuchu—ambaye sasa inadhihirika kuwa ndiye mke halali wa Diamond.

The post Diamond amuoa Zuchu, asema “Siku Ikifika Nitawaambia Ilivyokuwa” appeared first on Wasafi Media.



Prev Post Wanafunzi DIT, UDSM na UDOM Wapata Tuzo za Juu Nchini China
Next Post UN: Ni “Uhalifu wa Vita” kuzuia chakula kuwafikia Wapalestina wa Gaza
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook