Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

BAADA YA KUSHINDWA KUBEBA NDOO CAF….JULIO ‘AWANYOSHEA KIDOLE’ MABOSI SIMBA…

  • 36
Scroll Down To Discover

KOCHA Msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars, Jamhuri Kihwelo “Julio”, amewataka viongozi wa klabu ya Simba wanaingia sokoni kusajili wachezaji wa kiwango cha juu kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Julio amesema kuwa ili Simba waweze kushindana vikali dhidi ya vigogo wa soka Afrika kama Al Ahly na RS Berkane, wanahitaji kuimarisha kikosi chao kwa kusajili wachezaji wenye ubora wa hali ya juu, watakaoweza kuleta ushindani mkubwa katika mechi za kimataifa.

“Kwa sasa timu zetu zinazoshiriki michuano mikubwa ya kimataifa zinapaswa kufanya usajili wa maana. Hatuhitaji tu wachezaji wa ndani, bali wale ambao wanaweza kutufikisha mbali kwenye mashindano makubwa,” amesema.

Julio ameongeza kuwa licha ya Simba kuonyesha soka safi na kupambana kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane, walizidiwa na ubora wa wachezaji wa wapinzani wao.

“Simba walipambana, walicheza vizuri, lakini tofauti ya ubora wa wachezaji ilionekana wazi. Hili linapaswa kuwa somo kwa viongozi, kwamba kama tunataka kufika mbali zaidi, ni lazima tuongeze ubora wa kikosi,” amesema.

Kocha huyo pia ameonesha imani kuwa klabu za Tanzania sasa zimeanza kuwa na mawazo ya kushinda vikombe vya Afrika, na kwa mantiki hiyo, wanapaswa kuwekeza kwa kusajili nyota watakaosaidia kutimiza ndoto hizo.

“Ndoto ya kutwaa kombe la Afrika sasa ni ya kweli kwa timu zetu. Tunaweza kufika huko, lakini sharti ni kuhakikisha tunaleta wachezaji bora watakaoongeza nguvu kwenye timu,” amesema.

The post BAADA YA KUSHINDWA KUBEBA NDOO CAF….JULIO ‘AWANYOSHEA KIDOLE’ MABOSI SIMBA… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KISA FEI TOTO…..MO DEWJI, GSM KUTUNISHANA MSULI WA PESA…AZAM WAMPA DAU NONO ZAIDI…
Next Post WANAOTAKA KUTUSUA KIMATAIFA….HUU HAPA USHAURI WA MSUVA KWA MASTAA WA KIBONGO…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook