Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Serikali Yawataka Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuhakikisha Miradi Wanayosimamia Inakidhi Viwango

  • 4
Scroll Down To Discover

Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi na Umeme kutoka Wizara ya Ujenzi Mwanahamisi Kitogo akizungumza kwenye mahafali hayo.

SERIKALI imewataka Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi nchini kuhakikisha miradi wanayoisimamia inakidhi viwango ili kuwa mfano kwa vizazi vijavyo.

Pia imezindua vazi jipya la kitaaluma lililobuniwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB)litakalotumika katika kutekeleza majukumu katika sekta ya Ujenzi.

Vazi jipya lilivyozinduliwa.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi kwenye mahafali ya pili ya wataalamu waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi na Umeme kutoka Wizara ya Ujenzi, Mwanahamisi Kitogo alisema taaluma ya Ubunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi ni muhinu kwa mustakabali wa taifa.

Aliwataka wahitimu na wataalamu wa taaluma hiyo kuacha tabia ya kuchukua miradi bila kufuata kanuni, Sheria na taratibu kwani kufanya hivyo ni kosa.

Sehemu ya wahitimu hao.

“Hakikisheni mnakamilisha miradi mnayoisimamia kwa ukamilifu kwa maslahi ya jamii na taifa ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kwa kuchukua miradi bila kufuata kanuni na taratibu za kisheria,” alisema Kitogo na kuongeza kuwasisitiza kuhakikisha wanafanya kazi kwa haki.

Aliongeza kuwataka kuacha kufanya kazi kwa maslahi binafsi badala yake wahakikishe miradi wanayoisimamia inakidhi viwango.

Aidha amewasihi wataalamu wa sekta hiyo kuwa wabunifu kwa kubuni majengo ya kisasa zaidi ambayo yataibadilisha sura ya nchi na kuiwezesha kuwa kivutio kwa watalii wa ndani na nje.

“Acheni uvivu fanyeni vitu vya tofauti pale mnapobuni majengo ili yawe kivutio kwa watalii wa ndani na nje ya nchi,” alisema Kitogo na kuongeza kuwa haya yote yatawezekana kwa kutembelea nchi za wenzetu kuona na kujifunza mambo tofauti.

Mmoja wa wahitimu hao akipewa mwongozo wa kanuni za kazi.

Kwa upande wake Kaimu Msajili wa AQRB, Dkt. Daniel Matondo alisema jumla ya wahitimu 170 wamehitinu mafunzo maalumu ya bodi hiyo na kusajiliwa ili kuongeza idadi ya wataalamu kwenye sekta hiyo.

” Leo ni siku ya furaha na kumbukumbu, tunashuhudia juhudi za wahitimu 170 zikithibitishwa hadharani baada ya miaka ya masomo makini, mafunzo ya vitendo na mitihani ya kitaaluma.

Kwa sasa mmekamilika kama wataalamu walioidhinishwa kisheria mkiwa tayari kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa kupitia ujenzi wa miundombinu salama yenye ubora na tija,” alisema Dkt. Matondo

Alisema mahafali haya yana tija kwani yanatambua jitihada kubwa na nidhamu ya wahitimu hadi kufikia usajili, yanawahimiza wananchi na wadau wote kutumia wataalamu waliosajiliwa ili kulinda usalama, thamani ya fedha na ubora wa miradi ya ujenzi.

Akifafanua kuhusu vazi jioya la kitaakuma Dkt. Matondo alisema kitatambulisha rasmi wataalamu kwenye fani hiyo kama mavazi mengine ya kitaaluma wakiwepo madaktari wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Naye Mkurugenzi Usajili na Maendeleo ya Taaluma kutoka (AQRB) Bundala Robert alisema hadi kufikia Agosti 30 2025 bodi imesajili jumla ya wataalamu 1,708 na Makampuni 489 katika fani mbalimbali za ujenzi.

Alizitaja baadhi ya fani ambazo bodi imesajili wataalamu wake kuwa ni pamoja na Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi, Teknolojia ya Majengo, Usanifu wa ndabi ya jengo, na Ubunifu wa mandhari ya nje ya majengo.

Alizitaja zingine kuwa ni Umeme na Ujenzi, Utathmini Majengo na Umeneja Miradi ambapo alisema wataalamu hao kwa pamoja wana jukumu la kusanifu na kupanga majengo na mandhari kwa ubora, usalama na mazingira, kuboresha mipango miji na makazi kwa uendelevu sambamba na kusimamia ubunifu unaozingatia sera na kanuni za kitaifa.



Prev Post Wafanyabiashara 186 Wahitimu Mpango wa Maendeleo ya Usambazaji Bidhaa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook