
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, usiku wa Septemba 4, 2025, ameungana na maelfu ya waumini wa Kiislamu katika Maulid Makuu ya Kitaifa ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar.
Sherehe hizo ziliambatana na qaswida, dua, na mihadhara ya kidini iliyoeleza historia na mafunzo ya Mtume Muhammad (S.A.W), yakisisitiza mshikamano, amani na mshikamo wa kijamii.
Dkt. Mwinyi alisisitiza umuhimu wa kufuata maadili na mwenendo wa Mtume (S.A.W) katika maisha ya kila siku, akiwataka wananchi kuendeleza mshikamano wa kidini na kitaifa kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!