
Mgombea Mwenza wa CCM, Balozi Emmanuel Nchimbi, amehutubia kwa moyo mkunjufu wananchi wa Meatu, akisisitiza dhamira halisi ya Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuwaletea maendeleo ya kweli.
Ameeleza mafanikio yaliyoshuhudiwa tayari Meatu na miradi mikubwa iliyotekelezwa katika sekta mbalimbali, huku akiahidi kwa niaba ya Dkt. Samia kuwa safari ya maendeleo itakazidi kuimarika kupitia ahadi zilizomo kwenye Ilani ya CCM 2025–2030. Ahadi hizi, amesema, zitalenga moja kwa moja kuboresha maisha ya wananchi wa Meatu.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!