Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wekundu wa Msimbazi Wasogeza Tarehe ya Hafla ya Jezi Mpya

  • 5
Scroll Down To Discover

Klabu ya Simba SC imetangaza kusogeza mbele tarehe ya uzinduzi wa jezi zake mpya kwa ajili ya msimu wa 2025/26. Awali, hafla hiyo ilikuwa ifanyike Agosti 27, 2025, lakini sasa itafanyika Agosti 31, 2025.

Kupitia taarifa ya klabu, sababu za mabadiliko hayo hazijawekwa wazi, licha ya mashabiki wengi kusubiri kwa hamu tukio hilo kubwa la klabu hiyo ya Msimbazi.

Uzinduzi huo umepangwa kufanyika katika ukumbi wa SuperDome, Masaki, kuanzia saa 1:00 usiku. Shabiki atakayehudhuria hafla hiyo atatakiwa kulipia kiingilio cha Shilingi 250,000.

Tukio la uzinduzi wa jezi za Simba SC limekuwa likivuta hisia kila msimu kutokana na ubunifu wa mavazi hayo pamoja na mvuto wa hafla yake, ambayo mara nyingi huambatana na burudani na matukio maalumu yanayoshirikisha mastaa wa ndani na nje ya uwanja.



Prev Post CHADEMA Yamteua Gerva Lyenda Kuongoza Idara ya Habari
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook