Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

BAADA YA KUMALIZANA NA CHAN….TSHABALALA APEWA SIKU 5 YANGA….FOLZ HACHEKI NA MTU …..

  • 1
Scroll Down To Discover

KAMBI ya Yanga imezidi kunoga kule Avic Town, Kigamboni Dar es Salaam, lakini jana ilikuwa katika mapumziko flani mafupi na kazi itaendelea leo Jumatatu, huku kocha wa timu hiyo, Romain Folz akitoa msimamo mzito ambao mabosi wa klabu wameafikiana nayo.

Yanga iliamua kuahirisha safari ya kwenda Misri kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya baada ya kocha Folz kuvutiwa na mandhari ya Avic Town na fasta akaanza kulifua jeshi hilo ili kujiandaa na msimu mpya ikiwamo mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Septemba 16.

Katika kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa, kocha huyo aliamua kuwapa mapumziko maalumu mastaa watano walioko nje ya kikosi hicho.

Kuna wachezaji watano ambao hawako kambini Yanga ambayo Folz anaendelea kutengeneza timu, wakiwamo mabeki Ibrahim Abdullah ‘Bacca’, nahodha msaidizi, Dickson Job, beki mpya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Clement Mzize.

Nyiota hao watano walikuwa katika kikosi cha Taifa Stars, kilichokuwa kinashiriki Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024, kilichoishia robo fainali iking’olew na Morocco.

Folz amewasiliana na mastaa hao kila mmoja kisha akawapongeza kwa kiwango bora walichoonyesha kwenye mechi hizo huku akiwatia kufuatia kutolewa.

Baada ya salamu hizo akawaambia anajua kila muda wa kila mchezaji aliotumika katika kikosi cha Stars pamoja na namna walivyotumika msimu uliopita, akiwa na rekodi zao zote.

Kocha huyo akawaambia mastaa hao kuwa anataka wapumzike akiwapa siku saba kila mmoja kutoka pale kambi ya stars ilipovunjwa kupata mapumziko kamili bila kufanya lolote zaidi ya mazoezi ya kawaida ya kushtua mwili.

Hata hivyo, Folz amewaambia mastaa hao, anajua itakuwa vigumu kwao kujiunga na kikosi chake kwasasa kwa kuwa kutakuwa na mchezo mmoja wa timu ya taifa kuwania kucheza Kombe la Dunia, mara baada ya ratiba ya mapumziko hayo kumalizika.

Kocha huyo amewaambia wachezaji hao kuwa watakutana mara baada ya mechi hiyo endapo wote wataitwa ambapo kama kutakuwa na atakayeachwa atajiunga haraka na kambi yao.

Tanzania itacheza dhidi ya Niger Septemba 9, nyumbani kuwania kucheza Kombe la Dunia utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

The post BAADA YA KUMALIZANA NA CHAN….TSHABALALA APEWA SIKU 5 YANGA….FOLZ HACHEKI NA MTU ….. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post YANGA ….CHANZO CHA SOWAH KUTOKUCHEZA DABI YA KWANZA MSIMU HUU…UKWELI HUU HAPA…
Next Post MASHINE MBILI MPYA SIMBA HIZI HAPA….’MAJAMAA’ YANAPIGA KAZI HATARI…..
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook