Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Taifa Stars Yaaga Chan 2024 Baada Ya Kupigwa Na Morocco

  • 4
Scroll Down To Discover

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeondolewa kwenye michuano ya CHAN 2024 baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Morocco katika mchezo wa robo fainali uliochezwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 65 kupitia kwa Lamlioui, na kuipa Morocco tiketi ya kutinga nusu fainali.

Kwa matokeo hayo, Tanzania inaungana na Kenya kutupwa nje ya michuano hiyo. Kenya walifungwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na Madagascar katika robo fainali nyingine.

Hivyo, Morocco imeungana na Madagascar kwenye hatua ya nusu fainali huku ikisubiri washindi wa michezo mingine ya robo fainali.

Matokeo ya Robo Fainali (CHAN 2024):

Tanzania 🇹🇿 0-1 🇲🇦 Morocco

Kenya 🇰🇪 3(3)-3(4) 🇲🇬 Madagascar



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 23, 2025
Next Post Rais Samia Amtembelea Dr. Mabodi Hospitalini Dodoma
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook