Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

NAFASI Za Kazi Pangani District Council

  • 10
Scroll Down To Discover

NAFASI Za Kazi Pangani District Council

NAFASI Za Kazi Pangani District Council

NAFASI Za Kazi Pangani District Council

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MSAIDIZI WA OFISI KWA MKATABA MIEZI MITATU (03)

Katibu Tawala Mkoa wa Tanga kupitia Ofisi ya Katibu Tawala Wilaya ya Pangani anawatangazia wananchi wote raia wa Tanzania wenye sifa za kuomba nafasi za kazi za Msaidizi wa Ofisi kwa Mkataba miezi Mitatu (03) kama ifuatavyo:-

✅MSAIDIZI WA OFISI NAFASI (04)
SIFA ZA MWOMBAJI.

  • Awe na Elimu ya Kidato cha nne (Form IV) aliyefaulu vizuri katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati. Wenye ujuzi wa kutumia Komputa, mafunzo ya mapokezi na upokeaji simu na cheti cha utunzaji Kumbukumbu watapewa kipaumbele.
  • Mwombaji awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai au kufungwa jela.
  • Mwombaji aandike barua yake ya maombi mwenyewe (kwamkono) na aambatanishe wasifu (CV), vivuli vya vyeti vyake vya taaluma na ujuzi, cheti cha kuzaliwa na picha mbili (Passport size).
  • Testmonials provision result, result slip kiapo cha kuthibitisha kuzaliwa HAVITAKUBALIKA.
  • Mwombaji awe tayari kufanya kazi katika mazingira ya vijijini kwa maana ya Ofisi za Maafisa Tarafa.
  • Mwombaji anatakiwa awe na umri usiozidi miaka 45.
  • Waombaji ambao waliwahi kuacha kazi, kuachishwa kazi au kufukuzwa kazi hawaruhusiwi kuomba isipokua kama ana kibali cha Katibu Mkuu kiongozi cha kuajiriwa upya.
  • Mwombaji anatakiwa asiwe na mkataba wa kikazi na Katibu Tawala Wilaya kwa sasa.

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kufanya usafi wa Ofisi na mazingira ya na ndani ikiwani pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo.
  • Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofisa wanaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
  • Kusambaza barua za ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
  • Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinawekwa sehemu zinazostahili.
  • Kufungua milango na madirisha ya ofisi wakati wa asubuhi na jioni nakuyafunga baada ya saa za kazi.
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.
  • Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.
  • Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa Maafisa/Ofisi watakapopewa huduma.
  • Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
    .Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka n.k) katika mafaili.

Maombi yote yaletwe ofisini kwa anuani ifuatayo:
Katibu Tawala Wilaya,
S. L. P. 31, PANGANI.

Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 10/09/2025 kabla ya saa 9.30 alasiri.

DONWLOAD PDF YA TANGAZO HAPA



Prev Post NAFASI Za Kazi DCB Commercial Bank PLC
Next Post NAFASI Za Kazi Gaini Company Limited (GCL)
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook