Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Samia Azungumza na Wananchi wa Ikungi, Atoa Ahadi Kuu za Maendeleo (Picha +Video)

  • 10
Scroll Down To Discover


Wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Ikungi Mashariki, wilayani Manyoni mkoani Singida, wamejitokeza kwa wingi leo Jumanne, Septemba 9, 2025, kushiriki mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akijinadi mbele ya mamia ya wananchi, Dkt. Samia aliahidi kuendeleza na kuongeza kasi ya miradi ya maendeleo ikiwemo kuanzisha kongani ya viwanda itakayoongeza thamani ya mazao na shughuli za kiuchumi ndani ya wilaya hiyo.

“Ndugu zangu kwenye ajira za vijana, awamu iliyopita tumefanikiwa kuleta kiwanda kimoja kikubwa, lakini tunajipanga kuja na kongani ya viwanda ndani ya wilaya hii, viwanda ambavyo vitaongeza thamani mazao yanayolimwa au shughuli zilizopo ndani ya wilaya hii,” alisema.

Aidha, Dkt. Samia alisisitiza kuwa wilaya ya Ikungi imepiga hatua kubwa katika upatikanaji wa nishati ya umeme, ambapo vijiji vyote 101 tayari vimeunganishwa na umeme, huku kazi ikiendelea kwenye vitongoji.

“Mbele tunakokwenda, mkitupa ridhaa, tunakwenda kumaliza kazi yote Tanzania nzima kila mtu awe na umeme,” aliongeza.

Kwenye sekta ya elimu, Dkt. Samia ameahidi kuendeleza sera ya elimu bure sambamba na kuongeza miundombinu ya madarasa ya shule za msingi na sekondari wilayani humo. Pia alitangaza mpango wa serikali ya CCM wa kujenga chuo cha ufundi ndani ya wilaya ya Ikungi ili kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa moja kwa moja utakaowaingiza kwenye ajira.

Mkutano huo ni sehemu ya kampeni za CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, ambapo Dkt. Samia anawania kuendelea kuongoza Tanzania kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.



Prev Post Utawala wa Kikatili Waanguka Nepal, Waziri Mkuu Mstaafu Apata Kipigo
Next Post Alipambana sana kupata mapenzi ya huyu binti bila mafanikio ila leo hii wapo pamoja
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook