Dar es Salaam bado inazungumza kuhusu tukio lililotikisa mitaa ya kifahari – Amarula Sundown Sessions, lililofanyika Jumapili, 7 Septemba 2025.
Ni wachache tu waliopata nafasi ya kuhudhuria, kwani tukio hili lilikuwa laini ya mwaliko maalum. Wageni waliokuwa ndani walihusisha majina makubwa ya burudani, influencers wenye nguvu mitandaoni na mastaa wa jiji waliokuja kushuhudia namna Amarula inavyoweza kugeuza jioni ya kawaida kuwa kumbukumbu isiyosahaulika.
Mandhari ya jioni ilitawaliwa na muziki wa hali ya juu, mapambo ya kiubunifu na vinywaji vya Amarula vilivyochanganywa kitaalamu. Kila kipengele kilionyesha ubora wa chapa hii – chaguo la watu wa hadhi, ladha ya premium na urithi wa Afrika.
Kwa waliohudhuria, ilikuwa ni nafasi ya kipekee kushiriki katika tukio ambalo halitokani na sherehe za kawaida, bali ni sehemu ya urithi wa Amarula kama chapa ya kimataifa yenye mizizi imara barani Afrika.
Kwa wale waliokosa, gumzo linaendelea: Amarula Sundown Sessions imeacha alama kama tukio lililoweka viwango vipya vya burudani jijini Dar.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!