Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wananchi Dar Watakiwa Kupaka Rangi Majengo Yao Kabla ya Septemba 30

  • 7
Scroll Down To Discover

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, ametoa agizo kwa wananchi wote jijini Dar es Salaam kupaka rangi majengo yao, hususan katika maeneo ya Kariakoo, Mchikichini, Jangwani, Kivukoni, Kisutu, Gerezani, Mchafukoge, Upanga Mashariki na Upanga Magharibi.

Agizo hilo limetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 3(1) cha Sheria, Sura ya 293 (marejeo ya 2023), na limeelekeza kwamba zoezi la upakaji rangi likamilike kabla ya Septemba 30, 2025.

Mabelya amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayeshindwa kutekeleza agizo hilo ndani ya muda uliowekwa.

“Dar es Salaam Yetu, Fahari Yetu – Tutunze Mazingira kwa Ustawi wa Jamii na Maendeleo Endelevu,” — inasema sehemu ya tangazo hilo.

VIDEO: TUNDU LISSU AFIKISHWA MAHAKAMA KUU AKIWA na MABEGI ya VITABU – AZINGIRWA na ASKARI MAGEREZA..



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 09, 2025
Next Post GUMZO LA JIJI. KWA SASA NI AMARULA SUNDOWN SESSIONS
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook