
Wananchi wa Nyororo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, wamemiminika kwa wingi kumpokea na kumpongeza Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipowasili eneo hilo tarehe 6 Septemba 2025 katika muendelezo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.
Katika mkutano huo wa hadhara, wananchi walimhakikishia Rais Samia kuwa tarehe 29 Oktoba 2025 haina kizuizi, kwani kura zao zote ni za kumrejesha madarakani. Viongozi wa kijamii na vijana walipaza sauti zao wakimthibitishia kuwa anaungwa mkono kwa dhati kutokana na kazi kubwa alizotekeleza katika kipindi chake cha uongozi.
Rais Samia, akihutubia wananchi, aliwashukuru kwa mapokezi makubwa na kuahidi kuendeleza sera na miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya Watanzania wote.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!