Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

DAWASA Yatoa Onyo: Mradi wa Usafi Mbezi Beach Kukamilika Bila Kusuasua

  • 1
Scroll Down To Discover

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire amemuagiza

Mkandarasi wa Mradi wa Usafi wa mazingira Mbezi Beach Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kuongeza nguvu ili kuukamilisha kwa wakati ili uanze kunufaisha Wananchi.

Utekelezaji wa mradi huo unahusisha uchimbaji na ulazaji wa bomba kwa umbali wa kilomita 101, ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma majitaka, ujenzi wa chemba 2,383 pamoja na mtambo wa kisasa wa kuchakata majitaka unaoendelea kujengwa eneo la Kilongawima ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 86.

Mhandisi Bwire ametoa maagizo hayo, alipotembelea mradi na kusema unaendelea vizuri lakini akimtaka mkandarasi kuhakikisha anaongeza nguvu zaidi ili uweze kukamilika muda uliopangwa.

“Hadi sasa kazi ya ulazaji wa mtandao wa mabomba kwa umbali wa KM 101 pamoja na ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma maji ipo mbioni kukamilika, lakini nimeridhishwa zaidi na kasi inayoendelea katika mtambo wa kuchakata majitaka ila niwasihi kasi hii iendelee ili mradi ukamilike kwa wakati na wananchi wanufaike,” amesema Mhandisi Bwire.

Kwa upande wa mkandarasi kampuni ya Beijing Construction Engineering Group, Mhandisi Lee Whan ameshukuru kwa ushirikiano kutoka pande zote zinazotekeleza mradi huo na kuhakikisha unatekelezwa na kukamilika kwa muda uliopangwa.

“Kwasasa kazi kubwa ipo katika ujenzi wa mtambo wa kuchakata majitaka, ujenzi umekwishaanza na unaenda kwa kasi, kazi ya usukaji wa nondo kwajili ya ujenzi wa mtambo inaendelea na kazi hii tunaifanya kwa nguvu kubwa tukilenga kukamilisha mradi kwa muda uliopangwa” ameeleza Mhandisi Whan.



Prev Post Iringa Yatikisika! Dkt. Samia Apokelewa Kwa Shangwe Nyororo – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook