

Afrika, Agosti 04, 2025: Xtelify, kampuni tanzu inayomilikiwa kikamilifu na Bharti Airtel (‘Airtel’) inayosimamia rasilimali na uwezo wote wa kidijitali wa Airtel, leo imezindua jukwaa la kisasa linalotumia AI ambalo limeandaliwa kwa ajili ya siku zijazo, ambalo litasaidia kampuni za simu duniani kuondoa ugumu wa kiufundi, kuelekeza nguvu kwa mteja, kuboresha uzoefu wa mtumiaji, kupunguza kuhama kwa wateja na kuongeza mapato kwa kila mtumiaji (ARPU). Suluhisho hili linashughulikia kila tabaka la mnyororo wa thamani wa mawasiliano, likiwa na injini ya data iliyojumuishwa kwa ajili ya maarifa na akili zinazotegemea AI kwa kiwango kikubwa; jukwaa la wafanyakazi kwa ajili ya kuratibu kazi kwa wakati halisi; na jukwaa la uzoefu kwa ajili ya kusimamia kila kipengele cha safari ya mteja kwa kampuni ya simu.
Xtelify imesaini ushirikiano wa kimataifa wa muda wa miaka kadhaa na wenye thamani ya mamilioni ya dola na Airtel Africa, ambapo Xtelify itatoa majukwaa yake ya program, yakiwemo Data Engine, Work na IQ. Utekelezaji wa Xtelify Data Engine na Xtelify Work utawawezesha wafanyakazi wa Airtel Africa wapatao 150,000 waliopo katika nchi 14 kupata maarifa ya soko kwa ajili ya mikakati inayolenga mahitaji mahususi na kuwezesha matumizi muhimu kama vile kulinda wateja dhidi ya spam na ulaghai katika bara zima la Afrika. Xtelify IQ itawezesha mawasiliano salama, ya wakati halisi na kwa njia mbalimbali, hivyo kuboresha ubora wa huduma na uzoefu wa mteja.
Jacques Barkhuizen, Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Africa, alisema, “Ushirikiano huu ni hatua ya mabadiliko makubwa katika dhamira yetu ya kujenga mustakabali wa kidijitali barani Afrika. Kwa kutumia majukwaa ya AI ya Airtel ambayo yameonyesha uwezo mkubwa nchini India, hatuboresha tu uendeshaji wetu bali pia tunaharakisha utoaji wa uzoefu unaolengwa binafsi kwa kila mteja. Zaidi ya hayo, huu ni mfano wa Airtel kutumia nguvu ya Airtel muunganiko wenye nguvu ambao utaendesha ukuaji endelevu, ubunifu, na thamani isiyo na kifani katika masoko yetu 14 ya Afrika.”
Binod Srivastava, Afisa Mkuu wa Biashara – Biashara ya Kimataifa, Bharti Airtel, alisema, “Tunafurahia kushirikiana na Airtel Africa. Kwa kuchanganya jukwaa letu bunifu la Xtelify na maono ya Airtel Africa, tutaendesha mabadiliko yao ya kidijitali na kukabiliana na changamoto ngumu zaidi za sekta kama vile kupambana na spam na ulaghai ili kuhakikisha ulinzi wa hali ya juu kwa wateja. Tunatarajia ushirikiano wa muda mrefu, tukifanya kazi pamoja kuweka viwango vipya kwa sekta hii.”
Xtelify pia imezindua jukwaa la wingu la kiwango cha kampuni za mawasiliano – ‘Airtel Cloud’. Jukwaa hili limebuniwa kushughulikia miamala milioni 140 kwa dakika kwa matumizi ya Airtel nchini India, na sasa linaenea kukidhi mahitaji yanayobadilika kila mara ya biashara nchini India. Likihifadhiwa katika vituo vya kisasa vya data vinavyotumia nishati endelevu, lenye utoaji huduma unaotegemea AI ya kizazi kipya, na linasimamiwa na wataalamu wa wingu 300 waliothibitishwa, Airtel Cloud ni jukwaa salama na la kuaminika linalotoa IaaS, PaaS na muunganisho wa hali ya juu, likihakikisha uhamiaji salama, upanuzi wa haraka, gharama nafuu na hakuna utegemezi kwa mtoa huduma mmoja.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!