Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mataifa 26 Yajitolea Kuunga Mkono Ukraine Kijeshi

  • 36
Scroll Down To Discover

Washirika 26 wa Magharibi wamejitolea rasmi kupeleka wanajeshi “nchi kavu, baharini au angani” kwenda Ukraine, siku moja tu baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kufikiwa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza.

Akizungumza baada ya mkutano wa kilele uliowakutanisha viongozi wa nchi 35, uliopewa jina la “Coalition of the Willing” (Muungano wa Walio Tayari), Macron alisema Marekani pia inatarajiwa kuidhinisha uungaji mkono kwa vikosi hivyo katika siku zijazo.

Rais Donald Trump, kwa upande wake, alidokeza kuwa msaada wa Marekani huenda ukaelekezwa zaidi katika usaidizi wa anga, jambo ambalo linahusiana na mazungumzo aliyoyafanya na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuhusu “ulinzi zaidi wa anga ya Ukraine.”

Hata hivyo, matumaini ya kupatikana kwa makubaliano ya kudumu ya amani yameendelea kufifia tangu Rais wa Urusi Vladimir Putin alipokutana na Trump mwezi uliopita huko Alaska.

Trump pia alisisitiza kuwa Umoja wa Ulaya (EU) unapaswa kushirikiana na Marekani kusitisha uagizaji wa mafuta na gesi kutoka Urusi, akisema hatua hiyo itasaidia “kusitisha kampeni za kivita za Urusi kwa njia za kiuchumi.”



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 06, 2025
Next Post Thailand Yampata Waziri Mkuu Mpya Baada ya Msukosuko wa Kisiasa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook