Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Bulaya na Matiko Waangushwa Mara Wabunge Wanaotetea Nafasi Zawaacha Mbali

  • 42
Scroll Down To Discover

Waliokuwa wabunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kisha kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ester Bulaya na Esther Mathiko, wameshindwa kuongoza katika kura maoni baada ya Wabunge wanaotetea nafasi zao Michael Kembaki wa Jimbo la Tarime Mjini na Robert Maboto wa Jimbo la Bunda Mjini, majimbo yote ya mkoani Mara, kuongoza kwa kura.

Esther Mathiko na Ester Bulaya walitia nia ya kugombea nafasi ya Ubunge kupitia CCM, na kisha majina yao kuwa miongoni mwa waliopendekezwa kupigiwa kura za maoni.

Mathiko ameshika nafasi ya tatu kwa kupata kura 196 huku Michael Kembaki anayetetea nafasi yake akipata kura 1,568.

Bulaya amepata kura 625 huku Robert Maboto anayetetea kiti chake akipata kura 2,545.



Prev Post Enock Koola Historia Imejirudia Jimbo la Vunjo!
Next Post TRA, NCAA, TANAPA NA TAWA KUUNDA KAMATI TENDAJI YA PAMOJA KUONGEZA MAPATO
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook