Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Davinci na Mocktail Syrups, Zasaini Mkataba na Frabby wa Kusambaza Bidhaa Uokaji keki

  • 29
Scroll Down To Discover

Mkurugenzi Mkuu wa Tartan Pastries in Bakery, Joan Severine ambaye pia ni Mkufunzi na Mbobezi wa masuala ya uokaji.

Dar es Salaam 31 Julai 2025: Kampuni ya Davinci, inayojihusisha na uzalishaji wa vinywaji vya Cocktail na Mocktail Syrups, imesaini mkataba wa makubaliano na Frabby Tanzania Ltd kwa ajili ya kusambaza bidhaa mbalimbali zinazotumika katika uokaji wa keki nchini.

Kupitia ushirikiano huo, kampuni hizo pia zimezindua bidhaa mpya ya Whipping Cream Powder, inayotumika kwa mapishi ya aina mbalimbali za keki, hasa katika upambaji na ujazaji wa bidhaa za uokaji.

Wadau katika picha ya pamoja.

Akizungumza Julai 31,2025 wakati wa hafla ya kusaini makubaliano hayo, Meneja wa Frabby Tanzania Ltd, Alexander Vitaris, alisema kuwa kampuni yake imejipanga kuhakikisha waokaji wa keki nchini wanapata malighafi bora na za kisasa zitakazoboresha shughuli zao za uzalishaji.

Meneja wa Frabby Tanzania Ltd, Alexander Vitaris (kushoto) na Mustafa Filiz wa Meneja biashara wa Kampuni ya Kerry Krater Export Sales and Business Development watengenezaji wa bidhaa za uokaji na utengenezaji wa keki. 

“Kupitia mkataba huu, sitawaangusha waokaji wa keki nchini. Tutahakikisha tunawapatia bidhaa bora na za ubunifu zitakazowasaidia katika utengenezaji wa keki,” alisema Vitaris.

Vitaris aliongeza kuwa atakuwa karibu na wadau wa sekta ya uokaji ili kuwapa mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya bidhaa mpya zitakazotolewa na kampuni hiyo.

Alisema mkataba huo pia utasaidia kuleta ladha na rangi mpya zinazotumika katika utengenezaji wa keki, lengo likiwa ni kuvutia wateja zaidi kupitia ubunifu wa bidhaa mpya kama Whipping Cream Powder.

Pia alibainisha kuwa ushirikiano huo utaongeza chachu katika uzalishaji wa vinywaji vya Cocktail na Mocktail kwa kuimarisha upatikanaji wa malighafi bora.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tartan Pastries in Bakery, Joan Severine, ambaye pia ni Mkufunzi na Mbobezi wa masuala ya uokaji pia alishiriki katika hafla hiyo, alisema kuwa mkataba huo utaleta manufaa makubwa kwa Watanzania waliopo katika sekta ya uokaji, hasa katika uzalishaji wa keki na vitafunwa mbalimbali.

“Nipo hapa kushuhudia matumizi ya Whipping Cream na namna inavyoweza kunisaidia katika bidhaa zangu za bakery. Bidhaa hii ni ya kipekee kwani ipo katika mfumo wa unga lakini ina kiwango kikubwa cha mafuta ambayo, inapopigwa, hutoa uzito unaofaa kwa mapambo ya keki na ujazaji wa bidhaa za uokaji,” alisema Joan.

Aliongeza kuwa bidhaa hiyo itaongeza ufanisi katika mazingira ya joto kwani inadumu kwa muda mrefu na hivyo kuwapa waokaji unafuu mkubwa katika kazi zao za kila siku.

“Niko tayari kutumia Whipping Cream hii katika bidhaa zangu mbalimbali za uokaji kwa kuwa nina imani itaongeza ubora na mvuto kwa wateja,” alisisitiza.



Prev Post Rais Samia Atembelea Tawi Jipya la NBC Ubungo Akizindua Rasmi Kituo Cha Biashara Kimataifa
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 02, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook