
Msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni za Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara, Jabir Shekimweri, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, amemtangaza Regina Ndege kuibuka mshindi baada ya kupata kura 891 kati ya zaidi ya kura 1,000 zilizopigwa.
Uchaguzi huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Manyara, ukihusisha wagombea mbalimbali waliowania nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika Bunge kupitia nafasi za Viti Maalum kwa wanawake.
Katika nafasi ya pili aliibuka Yustina Rahhi aliyepata kura 703, akiibuka mshindani wa karibu zaidi wa Regina Ndege.
Orodha ya Wagombea Wengine na Kura Zao:
Senorina Yunus – 214
Joyclen Umbulla – 168
Loema Peter – 90
Paulina Nahato – 71
Schola Mollel – 37
Anna Shinini – 23
Wagombea waliopata kura chache sasa wanabaki kusubiri mchakato wa mwisho wa vikao vya juu vya CCM vitakavyopitisha jina la mwisho la mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!