

RUKWA – Katika mchakato wa kura za maoni za Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Rukwa, Silvia Sigula ameibuka mshindi kwa kupata kura 494, akifuatiwa na Jacqueline Mzindakaya, kada maarufu wa CCM mkoani humo, aliyepata kura 434.
Kwa mujibu wa utaratibu wa CCM, nafasi ya kwanza na ya pili kwa kura za maoni kupitia UWT katika mikoa hujipatia nafasi ya kuteuliwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum, hivyo wawili hao wanatajwa kuwa washindi wa tiketi ya ubunge kupitia mkoa wa Rukwa kwa uchaguzi mkuu wa 2025.
Matokeo Kamili ya Wagombea 8 ni kama ifuatavyo:
Silvia Sigula – 494
Jacqueline Mzindakaya – 434
Bupe Nelson – 220
Agripina Mizinga – 173
Annastela Malaji – 85
Lucy Herman – 17
Dorice Bakari – 15
Agatha Daniel – 11
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!