Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

CCM Yapendekeza Marekebisho Madogo ya Katiba Kuboresha Mchakato wa Kura za Maoni – Video

  • 37
Scroll Down To Discover

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimependekeza marekebisho madogo ya Katiba yake ya mwaka 1977 (toleo la Mei 2025), ili kutoa mamlaka kwa Kamati Kuu ya chama hicho kuongeza idadi ya wagombea wanaoruhusiwa kushiriki katika hatua ya kura za maoni katika nafasi za ubunge, udiwani na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Mapendekezo hayo yamewasilishwa rasmi mbele ya wajumbe wa Mkutano Maalum wa CCM uliofanyika kwa njia ya mtandao siku ya Jumamosi, ambapo Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameeleza kuwa mabadiliko hayo yanalenga kuboresha mfumo wa uteuzi wa wagombea kwa kuzingatia mazingira halisi ya kisiasa kwenye maeneo mbalimbali.

“Mkutano wetu wa leo una ajenda moja tu – kupendekeza marekebisho madogo sana kwenye Katiba yetu. Hatukuona busara Kamati Kuu kujipa mamlaka yenyewe bila kurudi kwenu kwa sababu hiki ni chama cha WanaCCM wote, si cha Kamati Kuu pekee,” amesema Dkt. Samia.

Akisoma mapendekezo ya marekebisho, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Idara ya Oganaizesheni, Issa Haji Ussi Gavu, ameeleza kuwa marekebisho yanahusu Ibara ya 105(7F) ya katiba ya CCM ambapo inapendekezwa kuongeza maneno “isipokuwa kama Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itaamua vinginevyo”. Hii inatoa ruhusa kwa Kamati Kuu kuongeza idadi ya wagombea wa ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaoruhusiwa kushiriki kura za maoni katika kila jimbo, kulingana na mahitaji.

Aidha katika Ibara ya 91(6C) ambayo inahusu uteuzi wa wagombea wa udiwani nayo inapendekezwa kurekebishwa kwa mtiririko huo huo, ili Kamati Kuu iwe na uwezo wa kuruhusu zaidi ya wagombea watatu kupigiwa kura za maoni katika kila kata au wadi.

Baada ya mapendekezo hayo kuwasilishwa, Mwenyekiti Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa ufafanuzi akisisitiza kuwa lengo kuu ni kuongeza ushindani na kutoa nafasi kwa wanachama wengi zaidi kushiriki mchakato wa kidemokrasia wa kura za maoni.

Mabadiliko hayo, kwa mujibu wa Katiba ya CCM, yatapitishwa rasmi endapo yatapata uungwaji mkono wa theluthi mbili ya wajumbe wote wa Mkutano Mkuu. Wakati naaandika makala haya, taarifa zilisema ilipitishwa.



Prev Post CCM Yapitisha Marekebisho ya Katiba kwa Kishindo – Video
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JULAI 27, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook