Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Infinix Hot 60 Pro+ Inakuja na Wembamba wa 5.59mm, Kuweka Rekodi ya Kipekee

  • 44
Scroll Down To Discover

Kampuni maarufu ya kuzalisha simu janja duniani ya Infinix inatajwa kufanya mageuzi makubwa katika toleo lao jipya la simu aina ya HOT60 Pro+ ambayo itakuwa na wembamba wa 5.59mm na kuwa yakwanza yenye muonekano huo katika simu zilizo na muundo wa 3D Curved.

Taarifa mbalimbali zilizochapishwa na tovuti maarufu zinazohusu maswala ya Teknolojia ikiwemo Gsm Arena zimeeleza kwamba Infinix Hot60 Pro+ sio tu itakuwa na wembamba wa 5.59mm lakini pia itakuja na rangi nyingi za kuvutia watumiaji wao.


Bado haijaelezwa kwa undani simu hii itakuwa na mambo yapi mengine ya kuvutia ukiacha wembamba na rangi lakini tetesi zaidi zinaeleza kwamba simu hiyo itakuwa pia na Betri linaloweza kukaa na chaji kwa muda mrefu.

Kwa hapa Tanzania tayari Infinix kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wameshafungua milango kwa wateja wao kufanya Pre-Order ya simu hiyo kupitia link maalumu inayopatikana katika kurasa zao.



Prev Post Serikali Yachukua Hatua Dhidi ya “Cutting Master” kwa Kuwahusisha Watoto Katika Maudhui ya Kingono
Next Post Rais Dkt. Samia Ashiriki Ufunguzi Wa Kanisa La Arise & Shine Kawe Dar -Live Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook