Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mkutano Mkuu wa TAMWA 2025: Usawa, Heshima na Siasa Safi

  • 35
Scroll Down To Discover

Mwasisi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania(TAMWA) Edda Sanga

Mwasisi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania(TAMWA) Edda Sanga amesema Rais Samia Suluhu Hassan ni rais wa kwanza mwanamke ambaye Tanzania inajivunia kuwa na kiongozi wa juu mwanamke.
Amesema udhalilishaji unaofanywa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya wanawake wanasiasa, unajenga taswira kuwa mwanamke hafai katika ngazi ya uongozi.

“Kama udhalilishaji huu unakwenda hivyo unavyokwenda, bado tutaendelea kumuona mwanamke hafai katika ngazi ya uongozi ambayo sio sahihi, kwa sababu tumepigania kwa miaka yote huu kuona mwanamke anafaa kuwa pale,”amesema Sanga
Sanga ameyasema hayo katika mahojiano maalum wakati TAMWA kikitarajia kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka Juni 27 na 28 mwaka huu ambao unakwenda na kauli mbiu isemayo; “Tunajenga Tanzania ya heshima, usawa na siasa safi bila kejeli”

Mwasisi huyo wa TAMWA ambaye pia amewahi kuwa mwanahabari wa kituo cha Habari cha Taifa (TBC) zamani Radio Tanzania(RTD) amesema, kuna haja ya jamii nzima kuelimishwa jinsi ambavyo udhalilishaji huu unavyoathiri juhudi za asasi za kiraia, zilizofanywa na TAMWA ikiwamo, kuhakikisha mwanamke anapewa sura ya mama, mama mwenye maadili, mama anayeongoza familia.

“Tukubaliane kuwa kudhalilishwa kwa mwanamke mmoja, ni kudhalilisha jamii na ni kudhalilisha Watoto, basi jamii ikubali kuwa hili ni suala linalotakiwa kupewa uzito wa hali ya juu, na vyombo vya Habari vihakikishe yale mabaya yasionyweshe,” amesema na kuongeza:
“Sisi tulio katika vyombo vya habari tunapoona mambo haya yanaonyeshwa kweli tunajisikia vizuri?. Je ni sahihi kuruhusu vitu kama hivyo viende, si sahihi?”

Amezungumzia nguvu ya mitandao ya kijamii na jinsi inavyotumika kusambaza chuki mitandaoni na kusema, iwapo mitandao ya kijamii inatumiwa kusambaza ajenda kuwa eti kuwa mwanamke rais ndio mbaya kuliko wote, mbona tumeona wanaume wanafanya mabaya kuliko hayo tunayoyaona, na bado wapo madarakani?

“Kama kuna makosa, tusahihishe kwa namna ambayo ni chanya, kwa kujenga hoja na sio kwa namna hasi na katika kuharibu, unadhani unamharibia mmoja kumbe unaharibia taifa, kwa hiyo inakwenda kuleta taswira mbaya kwa taifa zima,” amesema
Kwa mwaka huu, Mkutano Mkuu wa TAMWA unafanyika chini ya kauli mbiu isemayo, “Pinga Lugha za Matusi na Kejeli Dhidi ya Wanawake Katika Siasa.” Kauli mbiu hii inalenga kuchochea mjadala mpana na kuibua mikakati madhubuti ya kupambana na matumizi ya lugha za kudhalilisha, kubeza au kuwatisha wanawake wanaojihusisha na siasa, hali ambayo bado ni changamoto kubwa inayowarudisha nyuma wanawake wengi katika uongozi.

TAMWA inaamini kuwa vyombo vya habari vina nafasi ya kipekee katika kubadili mitazamo potofu na kuhimiza maadili na heshima katika majukwaa ya kisiasa.

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.



Prev Post Yanga Yaipiga Simba, Yabeba Ubingwa
Next Post Nilidhani Bosi Wangu Ananichukia Kumbe Adui Yangu Halisi Alikuwa Rafiki Yangu wa Karibu
Related Posts
© Image Copyrights Title

Yanga Yaipiga Simba, Yabeba Ubingwa

© Image Copyrights Title

BRELA yatoa msaada kwa Watoto wenye uhitajj

Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook