Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

KUELEKEA DABI YA JUNI 25…..WALIOPOTEZA TIKETI ZA DABI YA MACHI 8 ‘KUNYWENI MAJI’….

  • 32
Scroll Down To Discover

KIONGOZI wa N-Card Catherine Chami amewapa uhakika mashabiki waliopoteza tiketi zao ambazo walizikata kwa ajili ya mechi ya Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba iliyotakiwa kuchezwa Machi 8, 2025 bado wana nafasi ya kuingia uwanjani Benjamin Mkapa katika tarehe mpya iliyopangwa ya mechi hiyo Juni 25.

Akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa, N-Card wamejipanga kuhakikisha kuwa kila aliyekata tiketi basi ana nafasi ya kuingia uwanjani.

“Kwa wale ambao tiketi zilipotea basi wanaweza kufika katika ubalozi wa Ufaransa ili waweze kusaidiwa mapema kuepuka usumbufu siku ya dabi.

“Ila kwa upande wa wenye tiketi hawana shida kwani wataingia uwanjani kama kawaida kwa njia ya ‘kuswap’ kadi zao.”

Ofisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda alisema kuwa; “Bodi ya Ligi na timu mwenyeji zitaungana kuhakikisha kuwa mashabiki hawapati changamoto yoyote kwa wale waliokata tiketi.”

“Mashabiki watakaofika siku hiyo watapata faida mbili ya kwanza kushuhudia dabi na pili kuiona fainali ya bingwa wa Ligi Kuu Bara.”

The post KUELEKEA DABI YA JUNI 25…..WALIOPOTEZA TIKETI ZA DABI YA MACHI 8 ‘KUNYWENI MAJI’…. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KUHUSU INONGA KUTUA YANGA…MABOSI WASHINDWE WAO TU….ISHU YAKE IMEKAA HIVI….
Next Post UTAMU WA CHAN 2024 HUU HAPA…UFUNGUZI TZ ,KWA MKAPA….ZANZIBAR NDANI…..
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook