MAGAZETI ya Leo Jumanne 27 May 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo.
Bw. Abdul-Razak Badru ameteuliwa kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).
Kabla ya uteuzi huu, Bw. Badru alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), anachukua nafasi ya Dkt. Elirehema Joshua Doriye ambaye uteuzi wake umetenguliwa na
Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Nyansaho alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!