Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Majaliwa: Serikali itaendelea kuwaunganisha wafanyabiashara wa Kitanzania na mataifa mbalimbali

  • 41
Scroll Down To Discover

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea na mikakati ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wa mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Japan ili kuwawezesha kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo katika mataifa hayo.

Amesema Serikali imekuwa ikifanya hivyo kwa kushiriki katika makongamano mbalimbali ya kimataifa ambayo yamekuwa yakiwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji ili kuongeza tija kubwa kwenye masuala ya biashara na uwekezaji.

Amesema hayo leo Mei 26, 2025 alipofungua kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii lililowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wafanyabiashara na wawekezaji wa Japan katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Westin, Osaka, Japan ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa Tanzania katika maonersho ya World Expo Osaka 2025.

“Tumewaeleza wafanyabaishara na wawekezaji hawa wa Japan fursa ambazo zipo nchini, hii ni mara ya tatu tunakutana na wafanyabara na wawekezaji kutoka Japan, tayari tumeanza kuona manufaa ya makongamano haya kutokana na kuongezeka kwa biashara kati ya mataifa haya mawili,” amesema.

Waziri Mkuu amesema hadi Machi 2025 jumla ya makampuni 24 kutoka Japan yamewekeza nchini Tanzania katika miradi mbalimbali yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 42.70 nchini na kuwawezesha jumla ya Watanzania wapatao 1,182 kupata ajira.

Majaliwa amesema licha ya uwekezaji wa makampuni hayo, Serikali ya Tanzania imeendelea kunufaika na ushirikiano wake na Serikali ya Japan kwa kupata misaada katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo na miundombinu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameshuhudia utiaji saini wa hati sita za ushirikiano ikiwemo ya ushirikiano katika kuendeleza sekta ya mafuta baina ya Serikali ya Tanzania na Shirika la JGC la Japan, hati nyingine ni baina ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Axcel Afrika kwa ajili ya kukuza uwekezaji nchini.

The post Majaliwa: Serikali itaendelea kuwaunganisha wafanyabiashara wa Kitanzania na mataifa mbalimbali appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post Marekani Yamkamata Mtu kwa madai ya kujaribu kulipua ubalozi wake huko Israel
Next Post Dkt. Samia Suluhu Hassan Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu ya CCM
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook