
Papa Leo XIV apokea Pete ya Mvuvi kutoka kwa Kardinali Luis Antonio Tagle, Pro-Prefekti wa Dikasteri ya Uinjilishaji, wakati wa Misa ya Uzinduzi wa upapa wake katika Uwanja wa Mtakatifu Petro leo Jumapili, Mei 18.
Kama vile Petro anavyojulikana kama Mtume Mvuvi, pete hiyo inajulikana kama Pete ya Mvuvi, au Pete ya Uvuvi (Piscatory Ring), ikimaanisha mwendelezo wa safu ya mapapa kuanzia Papa wa kwanza hadi leo.
Papa anapofariki, Pete yake ya Mvuvi, pamoja na Muhuri wa Risasi, hupasuliwa kwa patasi, hivyo kuhakikisha kuwa muhuri huo hauwezi kughushiwa.
Kila pete ni ya kipekee na binafsi kwa kila Papa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!