Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Nusrat Hanje Kutangaza Kuhamia CCM, Aeleza Sababu za Kuachana na Chadema

  • 41
Scroll Down To Discover

Mbunge wa Viti Maalum kundi la Vijana kutoka Mkoa wa Singida, Nusrat Hanje

Mbunge wa Viti Maalum kundi la Vijana kutoka Mkoa wa Singida, Nusrat Hanje, ametangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) muda wowote kuanzia sasa ndani ya mwezi huu wa Mei 2025, ikiwa zimesalia siku chache kuelekea Bunge kuvunjwa.

Hanje ametoa wito huo Jumapili ya Mei 18, 2025, wakati akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara alioufanya viwanja vya Stendi ya Zamani, Ikungi Mjini.

Ameeleza kuwa chama chake pendwa ambacho amekitumikia kwa muda mrefu, ambacho ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amedai kuwa kwa sasa kimepoteza mwelekeo.

Amesema uamuzi huo wa kuhamia CCM ameufanya bila shinikizo lolote, bali ameamua yeye mwenyewe baada ya kuona na kuridhishwa na mambo makubwa ya kimaendeleo anayoyafanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa wananchi wa Singida na Tanzania kwa ujumla.

Katika mkutano huo pia, Hanje amewataka wana Ikungi kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono pale atakapokuwa amehamia CCM na kuwaomba wanachama wa CCM kumpokea na kumtuma kama wataona inafaa.



Prev Post Majaliwa Atoa Wito wa Amani na Ushirikiano Kwimba, Aahidi Maendeleo kwa Wote
Next Post Rais Dkt.Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook