Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

CCM Yatangaza Rasmi Ratiba ya Vikao vya Uteuzi wa Wagombea Wabunge

  • 3
Scroll Down To Discover

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza ratiba ya vikao vyake vya kitaifa ambavyo ajenda kuu itakuwa ni uteuzi wa wagombea Ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge wa Viti Maalum, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum.

Vikao hivyo vitafanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Agosti 17, 2025 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Gabriel Makalla, kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kimepangwa kufanyika tarehe 21 Agosti 2025, kikifuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kitakachofanyika tarehe 23 Agosti 2025.

Aidha, imeeleza kuwa vikao hivyo vyote vitafanyika jijini Dodoma

https://youtu.be/AJRQuE6pjmM



Prev Post Sababu ya Ndoa za Sasa Kuvunjika Mapema
Next Post Polisi Pwani Wakamata Watu 10 kwa Njama za Uhalifu Kibaha – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook